SULUHU YA KWELI NI KUKAA KWENYE KITI NA MEZA: MCHUNGAJI HANANJA

Na Jumanne Magazi 

09.06.2025

Dar es salaam 

Mchunga Richard hananja amelaani vitendo vya viongozi wa dini kutumia majukwaa ya dini ili kupataa umaarufu, katika swala la utekaji au kupotea kwa watu nchini.

Akizungumza na wanahabari hii leo juni 9,2024 jijini dar es salaam amesema hakuna dini wala mtu anayependezwa na vitendo watu kutekwa au kupotea, serikali na wahusika wanapaswa kutoa suluhu ya kweli ambayo itapatikana katika vikao halali.

Hananja amesema kwa siku za HIVI karibu kumeibuka kwa wimbi la viongozi wa dini kutumia nafasi zao kuishutumu serikali na vyombo vya ulinzi kuwa havitimizi wajibu WAO jambo ambalo amesisitiza kuwa sio kweli.

Amesema Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DKT SAMIA suluhu Hassan anaumizwa na inayoendelea ambapo amewaasa Watanzani kuaepuka mtego wa kujiingizwa kwenye mambo ya naweza kuwaingiza kwenye vurugu.

Aidha mchungaji ananja amehoji kila mara wakati taifa linapoelekea kwenye uchaguzi ndio huibuka baadhi ya watu kuanza kuleta chokochoko zinazowapa baadhi ya watu manufaa yao kisiasa, jambo ambalo linahatarisha amani na usalama wa nchi.

Katika hatua nyingine mchungaji hananja amesema Kuna haja ya kila pande zinazohusika kukaaa mezani kwani hata vitabu vya dini vinahimiza kutumia kiti na meza kujadili maswala yanayohusu jamii au taifa kwa ujumla.


 

Powered by Blogger.