SERIKALI YAHAMASISHA WANANCHI KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Juni 23, 2025 alifanya ziara katika bustani ya wanyamapori ya Tabora, maarufu kama Tabora ZOO, kwa lengo la kukagua na kuona usimamizi wa bustani hiyo ambapo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania hususani wa ukanda wa magharibi, wakazi wa Mkoa wa Tabora na Mikoa ya jirani kutembelea kivutio hicho cha kipekee ambacho kipo Katikati ya Mkoa wa Tabora.
Katika ziara hiyo, Dkt. Abbasi ameonesha kuridhishwa na uwepo wa bustani hiyo ambayo ni hazina ya vivutio vya wanyamapori na mazingira asilia. Ameeleza kuwa Tabora ZOO ni sehemu muhimu ya utalii wa ndani ambayo Serikali imejipanga kuhakikisha inafanya maboresho makubwa ya miundombinu ili kuvutia watalii wengi zai
di.
Hii ni Hifadhi ya kipekee, kuwa na eneo la heka zaidi ya 27 Katikati ya Manispaa ya Tabora au mji ni jambo kubwa, kwahiyo niwaombe wakazi wa Tabora, hii ni Johari yenu, ni bustani iliyowekwa Kwa ajili yenu mje kupumzika, kujifunza lakini si tu wakazi wa Tabora bali pia wanafunzi wa vyuo mbalimbali na watu wa ukanda huu tunawakaribisha sana," alisema Dkt. Abbasi.
Aidha, Katibu Mkuu huyo ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha bustani hiyo kwa kuongeza miundombinu ikiwemo sehemu za watalii kupumzika na burudani kama michezo ya watoto, maeneo ya chakula, vinywaji pamoja na kuongeza Idadi ya wanyamapori na mabwawa ya maji ili kuongeza mvuto zaidi kwa watalii.
Tabora ZOO ambayo ni mojawapo ya bustani chache za wanyamapori nchini zilizopo katika maeneo ya miji imeendelea kuwa kivutio cha kipekee Kwa watalii kutokana na mandhari nzuri na mazingira tulivu ambavyo vinaiweka bustani hii katika nafasi ya juu Kwa utalii wa mijini (Urban Wildlife Tourism).
Post a Comment