RC CHALAMILA,CAG WAWAFUNDA MADIWANI KINONDONI WAPONGEZA HATI SAFI MIAKA 4 MFULULIZO

Na Jumanne Magazi 

17.06.2025

Dar es salaam 

Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Albert Chalamila amewanasihi, na kuwashahuri, madiwani wa halmashahuri ya manispaa ya Kinondoni kuhusu kuanza kupanga mikakati bora ya  Ardhi kwa ajili ya matumizi ya kimkakati ili kuleta Maendeleo endelevu katika halmashahuri hiyo.

Ameyasema hayo hii leo wakati wa kufungwa kwa baraza la madiwani manispaa ya Kinondoni, ikiwa ni sehemu ya  kuhitimisha muhula wa miaka 5 ya baraza hilo, ambalo limehitimishwa hii leo 

Chalamila amesema kwa sasa muda umefika kwa baraza la madiwani Kinondoni kuanza kutenga maeneo maalum kwa shughuli za kiuchumi, ili kuwaletea Maendeleo wananchi wa Kinondoni kwa miaka mingi ijayo.

Akifafanua hilo chalamila amesema " kwa sasa amesema mkoa wa dar es salaam ni mkoa wa kiuhalisia ni mkoa muhimu kiuchumi kwani ndio kitovu uchumi nchini hivyo halmashahuri za mkoa huo zinapaswa kupanga ardhi kwa matumizi elekezi"

Aidha mkuu huyo amesema Dunia watu wanawekeza kwenye rasilimali ardhi hivyo amewashahuri madiwani na mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni kuanza mchakato wa kupanga maeneo ya viwanda,biashara,michezo,na vitega uchumi kwa ajili ya kuziletea halmashahuri fedha zitakazo endesha shughuli za Maendeleo alitoa mifano kwa nchi zilizo endelea.

Katika hatua nyingine chalamila amesema hivi sasa Kuna dalili ya maeneo mengi ya mkoa wa dar es salaam kugeuka kuwa, makaazi haramu yasiyopangwa jambo ambalo ni hatari kwa mustakabari mzima wa Maendeleo ya miji.

Awali mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG, Charles Kichele ameipongeza halmashahuri ya manispaa ya Kinondoni kwa kuwa na hati safi kwa kipindi cha miaka 4 mtawalia jambo ambalo linaleta faraja  kuona fedha za serikali zinazoletwa kwa ajili ya Maendeleo zinatumika ipasavyo kwa maslahi ya wananchi wote kwa ujumla.


 " Ni waziri ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali imekuwa ikifanya ukaguzi WA mara kwa mara hivyo na kubaini hati safi hivyo amempongeza mkurugenzi pamoja na madiwani wa Kinondoni kusimamia vyema fedha za serikali katika Maendeleo yaliyokusudiwa amesema CAG, Kichele.


Powered by Blogger.