DDI YAJA NA FARAJA CHUMBUNI MSAADA WA MBUNGE WAWAGUSA 1,200


 Mbunge wa Wananchi Jimbo la Chumbuni Mhe. Ussi Salum Pondeza amegawa sadaka ya sikukuu kwa kaya 1,200 zenye uhitaji, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kila mwaka kusaidia jamii katika mwezi wa Ramadhani na sikukuu za Iddi.

Msaada huo uliotolewa katika Chuo cha Utalii Maruhubi, ulijumuisha mchele, mafuta ya kupikia na pesa taslimu, na umelenga makundi maalum wakiwemo yatima na watu wasiojiweza.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu wa NEC  Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis, amesema viongozi wa CCM wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwahudumia wananchi bila kujiona au kubagua kama ilivyoelekezwa kwenye ilani ya chama.

Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wamemshukuru mbunge wao kwa moyo wake wa kujitolea, wakisema amekuwa karibu nao si kwa maneno bali kwa vitendo.

🗓️  05 June 2025

📍  Maruhubi - Zanzibar

Powered by Blogger.