WATANZANIA KATAENI UKATILI WA JINSIA
Na Jumanne Magazi
22.05.2025
Dar es salaam
Jamii imeshauriwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupiga vita matendo ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake, watoto na wazee, ambayo bado yanaendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mwezeshaji wa Stadi za Maisha kutoka Taasisi ya Elimu nchini, Rehema Longo, wakati wa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari kuhusu masuala ya ukatili, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Flaviana Matata.Rehema ametoa rai kwa jamii kutofumbia macho vitendo vya ukatili na kuripoti mara moja kwa mamlaka husika, badala ya kumalizana kienyeji. Pia amekumbusha kuwa endapo mtoto atafanyiwa ukatili, jamii inapaswa kutumia namba 116 kwa ajili ya msaada wa haraka.
Kwa upande wake, Afisa Miradi wa Flaviana Matata Foundation, Suzan Cleophas, amesema taasisi hiyo inalenga kufikia makundi yote nchini ili kukomesha ukatili unaokiuka haki za binadamu.
Post a Comment