UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME MBAGALA MBIONI KUKAMILIKA
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Kituo hicho Bw. Twange alisema kuwa Kituo hicho kimeongezewa uwezo mara mbili ya awali hivyo kitakuwa na uwezo mkubwa wa kusambaza umeme na kuondoa kabisa changamoto ya kukatika kwa umeme katika maeneo hayo.
Kituo hiki kimeongezewa uwezo mara mbili ya awali na mpaka sasa utekelezaji wa Mradi huu umefikia asilimia 70. Wananchi wa Mbagala na viunga vyake sasa wategemee umeme wa uhakika’’ alisisitiza Bw. Twange.
Pia, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Lazaro amemshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani milioni 6.4 ili kufanikisha Mradi huu wenye tija na manufaa kwa wananchi wa maeneo hayo na nchi kwa ujumla.
Kwa namna ya pekee tunaishukuru sana TANESCO kwa mradi huu, kwa awamu ya kwanza Mradi huu ulipaswa kujaribiwa mwezi Juni mwaka huu lakini Mradi umeweza kuonesha mafanikio kabla ya wakati kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa’’ alifafanua Mhe. Mapunda
Uboreshaji wa Mradi huu wa Kituo cha Kupokea na Kupoza na Kusambaza umeme cha Mbagala umegharimu Dola za Kimarekani milioni 6.4 ambapo sasa umefikia asilimia 70 ya utekelezaji wake na kukamilika kwake kunatarajia kusambaza umeme wa Megawati 165.
Post a Comment