DKT. MPANGO ASHIRIKI MAZUNGUMZO YA KISEKTA KANDO YA MKUTANO WA BODI YA MAGAVANA WA AfDB NCHINI IVORY COAST

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Akinwumi Adesina.

Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, unaoendelea katika Hoteli ya Sofitel Ivoire jijini Abidjan, nchini Ivory Coast.

Viongozi hao wawili wamejadili masuala mbalimbali yahusuyo maendeleo ya kiuchumi barani Afrika, hususan namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki hiyo, pamoja na fursa za uwekezaji na uboreshaji wa miundombinu.

Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa ngazi ya juu kutoka nchi wanachama wa AfDB kwa ajili ya kujadili mikakati ya kuendeleza bara la Afrika kupitia miradi ya maendeleo na uwekezaji endelevu.

Powered by Blogger.