COCA-COLA YAZINDUA PROMOSHENI MPYA YA "CHUPA LA MACHUPA" CHINI YA KIZIBO
09.04.2025
Dar es salaam
Kampuni ya vinywaji baridi ya a Coca Cola Tanzania, Leo hii imezindua kampeni mpya ya bahati nasibu inayojulikana kama "Chupa la machupa" chini ya kizibo ambayo itadumu kwa muda wa miezi miwili.
Aidha Nshimbo amesema kuwa kwakuwa kinywaji cha coca cola ni kinywaji cha muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiweka kumbukumbu zisizo za kusahaurika hivyo wamekuja na kampeni hiyo ya Chupa la machupa ili kurudisha kumbuka za aina mbali mbali kupitia Chupa ya coca cola ambapo sasa wataweza kujishindia zawadi mbalimbali, kupitia kampeni hiyo inakwenda kwa jina la chini ya kizibo.
Katika hatua nyingine Nshimbo ameeleza kuwa kwenye kipindi chote cha kampeni hiyo wateja wao wataweza kupata zawadi mbalimbali ikiwemo punguzo la bei hadi asilimia mia Moja huku kukiwa na punguzo la hadi Shilingi mia mbili kwa Chupa kwa muda wote promosheni hiyo ikiendelea.
Awali meneja mauzo wa coca cola Fatma mnaro amesema Kutokana na ushindani tuliopo hivi sasa kwenye soko wameona ni muda wao kama wadau wa vinywaji kuja na kitu cha kipekee ili kujaribu kushindana na chapa nyingine lakini pia kurudisha tabasamu na furaha kwenda kwa wateja wao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji Zaidi.Aidha mnaro amesisitiza kuwa "sisi kama coca cola, tumejizatito vya kutosha ili kuwapatia wateja wetu kilicho bora, nakuwa soda ya coca cola ni soda ya hali ya juu kulinganisha na soda zingine zilizopo sokoni kwa miaka mingi, ndani na Nje ya nchi.
Aidha amesema Kutokana na tafiti zinaonyesha kwa nchi nyingi barani Afrika maendeleo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku, hasa katika kukuza uchumi nchi husika kwa Zaidi ya asilimia 5 Pato la Taifa limekuwa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, hii ni kutokana na kuongezeka kwa mauzo"
Mapema ameitaja mikoa ambayo itanufaika na promosheni hiyo kuwa ni pamoja na Mbeya, Dodoma, Iringa, Dar es salaam, morogoro na kwingineko, hivyo amewaomba wateja wao kutumia kinywaji hicho ili kujishindia zawadi mbalimbali amesema Mnalo.
Post a Comment