NDUNGURU NDIO MSHINDI WA MIL 50 ZA MAGIFT YA KUGIFT DROO MWISHO.
Na Jumanne Magazi
13.2.2025
Kampuni ya mawasiliano ya Yas kupitia ofisi yake iliyopo manispaa ya Songea, imemzawadia Christian Nduguru mkulima na mfanyabiashara Songea mkoa wa Ruvuma kiasi cha Tsh Milioni 50 kama mshindi WA Promosheni ya Magift ya Kugift' Droo ya 12 na ya mwisho.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi hiyo, Meneja Biashara Yas Kanda ya nyanda za juu kusini Ronald Richard ameeleza kuwa wao kama Kampuni wamefanikiwa kukamilisha Shindano Hilo na hatimaye Leo bwana Nduguru ameibuka mshindi wa mil 50, ambapo anatoka kwenye kanda yake
Kampuni ya Yas kupitia kitengo cha Mixx by Yas imekuwa ikiendesha Promosheni hiyo ambayo ilianza mwishoni mwa mwaka Jana ambapo hadi kufikia Leo februari 13 Zaidi ya washindi 300 wameweza kujishindia zawadi mbalimbali, zikiwemo simu na pesa taslimu.
Kwa upande wake Mshindi wa zawadi hiyo bw Ndunguru, "amesishukuru kampuni ya Yas kwa kuchezesha Shindano Hilo ambapo amesema zawadi hiyo ni ya wanasongea wote kwani fedha hizo atazitumia ndani ya mkoa huo"
Aidha Ndunguru amesisitiza kuwa yeye kama Mteja mwingine amekuwa akishiriki mara nyingi kucheza ikiwa ni pamoja na kutuma miamala,kununua vitu mbalimbali kupitia Mixx by Yas na hatimaye Leo BAHATI imeangukia kwake amesema Ndunguru.
Kampuni ya Yas Tanzania kupitia kitengo cha Mixx by Yas imekuwa ikirudisha hisani kwa jamiii kwa kuchezesha kampeni mbalimbali Nchini ilikuwa karibu na Wananchi.
Post a Comment