NCHI ZA AFRICA ZINAWAJIBU WA KUTAFUTA SULUHU YA MZOZO WA CONGO

Na. Jumanne Magazi 

8.7.2024

Dar es salaam 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Amesema nchi za EAC na SADC hazipaswi kukaa kimya kwani zina wajibu wa kushughulikia mgogoro huu katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, unaogharimu maisha ya watu wasio na hatia.

Sote tunafahamu kwamba DRC bado inakabiliwa na migogoro, kama viongozi hatuwezi tukakaa kimya, jambo hili sio zuri, nchi zetu zina wajibu wa kuhakikisha tunashughulikia changamoto hii ambayo inaathiri watu nchini humo.

Ni muhimu kutafuta suluhisho la kudumu kwa pamoja kama wana jumuiya, kama mtetezi wa amani katika umoja wetu na nchi yangu ya Tanzania itaendelea kusaidia masuala ya kidiplomasia ili kumaliza mgogoro huu.

Rais wa Jamhuri ya Watu wa Kenya, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mhe. William Samoei Ruto

Mgogoro huu hautaweza kusuluhishwa kwa njia za kijeshi, lazima tukatae kupiga mabomu, ni suluhu za kidiplomasia ndizo zinahitajika kwa kushirikisha wadau mbalimbali. Mtakubaliana nami kuwa mazungumzo ya amani sio udhaifu bali ni kusikilizana na kushauriana.

Hatua za haraka zinahitajika ili kuinusuru DRC na watu wake, hii ni gharama kubwa, tunapaswa tuwaokoe mamilioni ya watu wanaohama kukimbia vita, matishio ya vifo, watoto wanahusishwa katika vikosi vya majeshi, tunahitaji kuchukua hatua kwani usalama wa nchi hiyo unaathiri dunia nzima na athari zake zinatakiwa zisipuuzwe.

Rais wa Zimbabwe na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Emerson Dambudzo Mnangagwa

Kinachoendelea nchini Congo kina madhara makubwa, sio kwa nchi hiyo tu bali kwa Bara zima la Afrika, hivyo nchi za Afrika zinatakiwa kushikamana kama kipindi cha enzi za kupigania uhuru ilivyokuwa.

Hali inayoendelea DRC na ongezeko la wahamiaji wa nchi hiyo lina madhara makubwa kwa Afrika, umoja wetu, mshikamano na undugu wetu vinatakiwa kufanikiwa sasa, tunatakiwa kishikamana, tuna jukumu la pamoja la kutatua changamoto za kiusalama tukizingatia tunu ya Kanda yetu na mkataba wa umoja wa Afrika, SADC na EAC. 
Katika mkutano huo maazimio yamependekezwa kupelekwa kwenye kamati maalum ambazo zitapitia mapendekezo na maazimio yote ya wakuu hapa ambapo baada ya mwezi mmoja watapleka kwenye mamlaka zingine kuona utekelezwaji wake.

Mkutano huo wa siku mbili ambapo awali hapo Jana mawazili WA ulinzi na mambo ya Nje walifanya kikao cha ndani kupendekeza Yale ambayo yanaonekana yanaleta Suluhu katika Mzozo huo wa mashariki kwa congo ambapo nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini imekuwa ikiishutumu  Rwanda kuwasaidia waasi wa M23.

Ambao hadi sasa wanadhaniwa kuwa wameshakamata sehemu kubwa ya mji WA Goma na maeneo mengine, huku dhamira ikwa ni kuelekea mji mkuu Kinshasa.

Tayari Serikali ya Congo imetangaza kuendelea na mapambano kutokomeza kundi Hilo ambalo linaonekana kuungwa mkono na mataifa mengine, Kutoka ndani na Nje ya Afrika.
 

Powered by Blogger.