MIXX BY YAS SASA KUFANYA KAZI BAHATI NASIBU YA TAIFA
Na Jumanne Magazi
28.2.2025
Dar es salaam
Kampuni ya bahati nasibu ya Taifa GBT Leo hii imeingia makubaliano ya ushirikiano na kampuni ya Mawasiliano ya YAS Tanzania, ushirikiano ambao utawezesha watazn kushiriki michezo ya kubahatisha kupitia Mixx by Yas.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa ITHUBA Tanzania Bw Kelvin Koka amesema “ BAHATI nasibu ya Taifa imeundwa kama rasilimali ya Taifa inayolenga kutoa thamani burudani na manufaa ya kiuchumikwa Wananchi wa Tanzania”Aidha amesema kuwa ushirikiano wa ITHUBA na Mixx by Yas ni uthibitisho wa dhamira yao katika kushirikiana na Taasisi zinazoheshimika na kushiriki yao kwa pamoja na Mixx by Yas .
Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika Leo Februari 28 jijini dar es salaam, ambapo amesema “ sisi kama ITHUBA tumejipanga kuhakikisha kwamba tunawaletea BAHATI nasibu watanzania ya Taifa ambayo itakuwa tofauti na zingine.
Vilevile Koka amesema kupitia ushirikiano huo wameweka misingi imara ya Bahati nasibu ya Taifa ili kuwaunganisha watu hatimaye kuleta msisimko,na kusaidia maendeleo kwa taifa kupitia michezo ya kubahatisha.
Kwa upande wake Bi. Angelica Pesha ameelezea furaha yake kuhusu ushirikiano huo, “Tunayo furaha kubwa kuwa sehemu ya mpango huu wa mabadiliko”
Amesema BAHATI Nasibu ya Taifa ni fursa adhimu ya kurahisisha watanzania kwa njia bunifu,kwa kutumia mifumo yetu ya kidigitali na suluhisho za kifedha,na tunawahakikishia wateja wetu wanapata huduma za Bahati Nasibu ya Taifa kwa nafuu na urahisi mkubwa
Aidha ushirikiano huo ambao imekuja na kauli mbili isemayo “ Amini, Cheza, Ushinde”
Post a Comment