CCM yachukizwa na vitisho vya ACT zbar
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuonya Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Zanzibar ,Omar Ali Shehe , na kumtaka aache kuwakaangia mbuyu wazanzibari kwa matamshi yake yenye vitisho .
Kadhalika CCM kimesema dalili za matamshi ya vitisho ma mikwara ni kielelezo ACT kimeshashindwa vibaya uchaguzi Mkuu wa Oktoba waka huu.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis huko akiwa katika wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba akifuatilia zoezi la Uandikishaji .
Mbeto alisema zoezi la uandikishaji Wapiga kura kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi Zanzibar, kila Mkaazi aliyeishi kwenye Jimbo moja kwa miezi 36, ndiye atakayekuwa mpiga kura halali si vinginevyo.
Alisema madai na kusema kuna wapemba 60 elfu wanye vyeti vya kuzaliwa Zanzibar lakini bado hawajaandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga kura, madai hayo hayana mashiko .
'Mwambieni Omar Shehe aache vitisho vya kitoto na kutisha wenzake. Sisi ni wanaume wenzake hivyo asitutishe mchana kweupe. Anayemtisha yuko wapi hadi atishike kwa maneno yake? " Alihoji Mbeto
Akitoa ufafanuzi zaidi , Mbeto alisema kutokea hitilafu katika teknolojia ya mitandao ni mambo ya kawaida, hivyo hicho si kigezo kwa ACT kutaka kulazimisha watu ambao si wakaazi , waandikishe kwa lazima na shuruti.
"Sheria inawakataza watu ambao si Wakaazi wa Jimbo husika kuandikishwa kwenye Daftari la Wapiga Kura .Ikiwa si Mkaazi usiyetambuliwa na Sheha wako hawezi kuandikishwa na kuwa mpiga kura" Alisisitiza Mbeto
Alieleza mtu anaweza kuwa na cheti cha kuzaliwa Zanzibar lakini asiwe si sifa ya kuwa mpiga kura endapo tu hana sifa si Ukaazi wa jimbo husika au jina lake halijaorodheshwa kwenye Daftari la sheha wa shehia .
"ACT kukubali ukweli hakina ubavu wa kuishinda CCM wakati Rais Dk Hussein Mwinyi ndiye mgombea wa urais Zanzibar. Othman Masoud hana sifa hata kimoja ya kumshinda Rais Dk Mwinyi aliyeiletea Zanzibar mageuzi ya kimaendeleo" Alisisitiza Mwenezi huyo
Hata hivyo Mbeto aliwataka wananchi ambao ni Wakaazi wa Zanzibar kwa mujibu wa sheria ya Ukaazi inavyoelekeza , wajitokeze kwa wingi ili kutumia haki ya kuandikishwa na kuwa wapiga kura .
"ACT wanataka kuidanganya dunia na kupotosha ukweli. Zanzibar kuna sheria ya Ukaazi inayomtaka mwananchi ili awe mpiga kura lazima awe amekaa jimboni kwa miaka mitatu "Alieleza Mbeto
Post a Comment