𝗨𝗩𝗖𝗖𝗠 𝗡𝗔 𝗕𝗢𝗗𝗔 𝗕𝗢𝗗𝗔 𝗪𝗜𝗟𝗔𝗬𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗡𝗢𝗡𝗗𝗢𝗡𝗜 𝗪𝗔𝗡𝗔𝗠𝗨𝗨𝗡𝗚𝗔 𝗠𝗞𝗢𝗡𝗢 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 2025
Akizungumza katika Mkutano huo Mgeni Rasmi Katibu wa Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ally Bananga amesema UVCCM na Maafisa Usafirishaji Wilaya ya Kinondoni wamefanya jambo kubwa na la Kihistoria la kumuunga Dkt Samia Suluhu Hassan kama Mgombea wa CCM 2025.
"Niwapongeze sana UVCCM Wilaya ya Kinondoni chini ya Mwenyekiti wenu Ndugu Abdulrahman Kassim na maafisa usafirishaji kwa Jambo hili kubwa la kumuunga mkono Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza Balozi Emmanuel Nchimbi kupeperusha Bendera ya CCM 2025".
Awali Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Abdulrahman Kassim alisema tukio hilo ni sehemu ya sherehe za kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi lakini pia kutimiza maazimio ya Baraza la UVCCM Wilaya ya Kinondoni ya kushirikiana na makundi mbalimbali katika Jamii kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka huu wa Uchaguzi Mkuu.Akizungumza kwa Niaba ya Maafisa Usafirishaji Mwenyekiti wa shirikisho la Bodaboda Wilaya ya Kinondoni amesema kwa kazi kubwa iliyofanywa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutekeleza miradi mingi mikubwa nchini, lakini pia kuwapunguzia faini kutoka shilingi 30,000 mpaka 10,000 kwa kosa moja hawaoni mbadala wake 2025 wao wanamuunga mkono na wataoziomba kura kwa ajili yake usiku na Mchana.
Mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe wa Baraza la UVCCM na Maafisa Usafirishaji wa Wilaya ya Kinondoni.
Post a Comment