MIXX BY YAS NA SOKO LA HISA DSE: ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO
Na Jumanne Magazi
29.1.2025
Kampuni ya mawasiliano Yas Tanzania pamoja na soko la hisa la Dar es Salaam DSE Leo hii 29 januari 2015, wamesaini Mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma ya kuuza na kununua hisa za DSE kupitia App ya Mixx by Yas
Makubaliano hayo ya kuuza hisa kupitia App ya Yas itawawezesha wateja wa Yas kununua hisa muda wowote ndani ya nje na hata nje ya nchi hatua ambayo imetajwa kuongeza ujumuishi wa huduma za kifedha na kukuza uchumi.Akizungumza wakati wa utiaji saini makubaliano hayo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yas, Innocent Rwetabura amesema wao kama Yas wanaendalea kufungua milango ya Fursa za uwekezaji kwa Watanzania wote.
"Asema kupitia huduma ya kuuza na kununua hisia kupitia App yetu ikiwa na lengo la kurahisisha kwa wateja wao kufanikisha Malengo Yao"
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji WA DSE, Peter Nalitolela amewataka wateja wa DSE kutumia mtandao wa Yas hususani huduma zinazotolewa ikiwemo Mixx by Yas,hivyo itawarahisishia wateja kupata huduma Bora Kutoka kwao kaka soko la hisa.
Aidha Nalitolela ameendelea kusisitiza kuwa wanayofuraha kuingia makubaliano hayo na Yas maana ni kampuni kubwa na yenye mafanikio hivyo kupitia makubaliano hayo DSSE inakwenda kupata mafanikio kupitia huduma ya App ya Yas.
Vilevile Nalitolela anasema wao kama DSE tayari "wanayo App yao hivyo kwa sasa kupitia App ya Mixx by Yas inakwenda kuongeza na kutanua ubora mkubwa katika soko la hisa la Dar es Salaam kupitia ushirikiano huo,kupitia simu zao za kiganjani" ili kuendelea kufanya uwekezaji kupita soko la hisa la Dar es salaam amema Nalitolela.
Awali Afisa mkuu wa Mixx by Yas Angelika Pesha amesishukuru DSE, kuichagua kampuni ya Yas hususani kupitia huduma ya Mixx by Yas ambapo amesema wako tayari kuhakikisha wanato huduma bora kwa soko Hilo la hisa ili kuwarahusishia wawekezaji WA ndani na Nje ya hisa kutimiza azma Yao ya kupata faida kupitia uwekezaji wao kupitia Mixx by Yas amesema Pesha.
Post a Comment