FUNDI GEREJI WA MADARE AIBUKA NA MIL 5 ZA MAGIFT YA KUGIFT DROO YA 11
24 .1.2025
Kampuni ya Mawasiliano ya Yas Tanzania Leo hii Januari 24, 2025, imekabidhi zawadi kwa washindi wa 5 Promosheni ya "Magift Kugift hii ikiwa ni droo ya 11.
Kampuni ya YAS Tanzania imekuwa Ikiendesha promosheni hiyo, kwa muda WA wiki 12 ambapo hadi kufikia Leo zaidi ya kiasi cha Shilingi Zaidi ya mil. 300, zimeshatolewa zikienda kwa washindi mbalimbali sambamba na zawadi hizo zikiwemo simu za mkononi.
Kwa upande wake mmoja wa washindi wa milioni Moja 1 wa wiki hii Herieth Charles Maimu, amesishukuru Yas kwa kuchezesha kampeni hiyo kwani imekuwa ikisaidia kuwapatia zawadi wateja wake ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyingine.
Naye Bi. Prescious stanlaus Mallya, amesema yeye ameibuka mshindi na hatimaye kipigiwa simu baada ya kufanya miamala mara kwa mara jambo lililopelekea kuibuka mshindi hivyo amewataka watanzania wengine kutumia mtandao wa Yas Tanzania kwani ni mtandao wenye huduma Bora na pia
Yas ikishirikiana na kitengo cha Mixx by Yas imekuwa Ikiendesha PROMOSHENI ya Magift ya Kugift ambapo wateja na washiriki wamekiri kuwa ni ya ukweli na uwazi na kuwa kila mtu anaweza kushida.Kwa upande wake Meneja wa Wateja maalum kutoka Mixx by Yas, Mary Lutha amewapongeza washindi WA Magift ya Kugift wa Droo ya 11 ambapo ametumia hafla hiyo kuwataka wateja wengine WA Mixx by Yas pamoja na Yas Tanzania kuendelea kushiriki Promoshe hiyo kwani kila mmoja ana fursa ya kujishinda zawadi hizo.
Kampuni ya Mawasiliano ya YAS inaendeshwa kampeni Promosheni hiyo, ambapo mshindi wa jumla anataraji kuondoka na zawadi ya gari ya pili aina ya Kia Sorante 0.kilometa wakati mshindi mwingine ataondoka na donge nono la Shilingi mil 50 katika droo siku ya mwisho.
Post a Comment