DAR IPO TAYARI KWA MKUTANO WA NISHATI BARANI AFRIKA :CHALAMILA

Na Jumanne Magazi 

9.1.2025

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert chalamila amesema ameridhika na maandalizi yanayoendelea kuelekea mkutano wa wakuu WA nchi barani Afrika, utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini dar es salaam.

Akizungumza wakati wa majumuisho ya Ziara yake aliyoifanye Leo Jan 9 2025,wakati akitembelea sehemu mbalimbali ikiwemo viwanja vya ndege, barabaraa na njia zitakazotumika wakati wa kupokesa ugeni huo.

Tanzania inataraji kuwa mwenyeji WA mkutano wakuu wa nchi za Afrika utakaozungumzia masuala ya Nishati ambao umepangwa kufanyika kuanzia januari 27-28 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano WA mwl Julias Nyerere jijini Dar es salaam.
Wakati WA Ziara hiyo Chalamila alitembelea uwanja WA ndege terminal   1 ambapo ameelekeza kupambwa kwa kuwekwa taa zipatazo 300.
Aidha chalamila amesema kwakuwa mkoa wa dar es salaam ndio mkoa mwenyeji mpango mikakati ni kuliweka jiji kuwa safi ambapo jumamosi wiki hii kutafanyika Zoezi la usafi kwa kuanzia na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana Wananchi wa mkoa huo kufanya usafi.
Katika hatua nyingine Chalamila ameagiza maroli yote yaliyopo kando kando ya barabara ya mwalimu Nyerere hadi posta mandera road,aidha chalamila pia amesema Katika kuhakikisha mkotano hup unakuwa WA aina yake nyumba Zaidi ya 10 zilizopo maeneo ya mjini yameanza kupakwa rangi ilikubadirk  muonekano wake.

Vilevile mkuu huyo wa mkoa amesema katika kuhakikisha nchi inakuwa kiuchumi kupitia mkutano huo mkubwa WA Nishati mpango WA jiji la dar es salaam ni kuanza kufungua taaa maeneo ya masoko makubwa yaliyopo katikati ya jiji ili kuanzia hivi karibuni Biashara ziwe zinafanyika masaa 24 kuanzia hivi karibuni.


Aidha mkuu WA mkoa pia amesisitiza kuwa Dar es salaam pamoja na Tanzania inakaenda kunufaika na mkutano huo kiuchumi na kiutamaduni kwani Wageni watakao kuja wanakwenda kutumia malighafii pamoja na huduma mbalimbali za nchi yetu hivyo ni faida kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla amesema Chalamila.

Powered by Blogger.