CCM :Miiaka 61 ya Mapinduzi Pemba imetia fora


Na Mwandishi  Maalum,Pemba 

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewashukuru wananchi  wa kisiwa cha Pemba  kwa kujitokeza kwa wingi mwanzo hadi mwisho kwa kushiriki kwao katika  uzinduzi wa miradi ya maendeleo na  kuhudhuria kwa wingi mikutano  ya hadhara ya Rais wa Zanzibar  Dk Hussein Ali Mwinyi .

Pia kimesema kushiriki kwao huko ni kielelezo  wananchi  wote wa pemba   wana imani kutokana na uchapakazi wa serikali  ya awamu  ya nane kwa kuimarisha  huduma jamii .

Pongezi  hizo zimetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Zanzibar  , Idara ya itikadi ,Uenzi na Mafunzo,Khamis Mbeto  Khamis, aliyesema ushiriki wa wananchi wa Pemba  mwaka huu umetia fora na kuvunja rekodi .

Mbeto  alisema  wananchi  hao bila kujali itikadi za kisiasa, walijitokeza kwa wingi kila walipoitikia wito wa  chama na serikali wa kuhudhuria shughuli  muhimu za  uzinduzi wa miradi ya kimaendeleo  .

Alisema wananchi  wa Mikoa miwili ya Kusini na Kaskazini Pemba,wakaazi wote  katika   Wadi  ,Majimbo na Wilaya za mikoa miwili ya pemba, hawakuona muhali badala yake wamekuwa mstari wa mbele   kuonyesha  upendo  ,hisia na furaha  zao

"Ni   sherehe  za  aina yake  za miaka 61 ya Mapinduzi. Pemba imetia fora .Wananchi wamehudhuria shughuli  zote za unzishaji na uzinduzi wa miradi  ya maendeleo  .Pia wamejitokezw kwa wingi  katika  kilele cha maadhimisho Uwanja wa Gombani ' Alisema Mbeto 

Aidha  alisema ni wazi kuwa wananchi  wameridhishwa na utendaji wa smz awamu ya nane,  unaojali maslahi  ya umma,utekelezaji wa mirdi na ahadi za serikali ulioondosha kero  zilizokuwa zikiwakabili wananchi.

"Imani siku zote  huzaa imani. Nyota njema huanza kuonekana mapama asubuhi . Wananchi wa Pemba kwa  kumuunga kwao mkono Rais  Dk Mwinyi ameahidi kuwalipa  utumishi uliotukuka" Alisema mwenezi huyo.

Mbeto  aliwataka wananchi  wa Zanzibar kuanza kutafakari na kupuuza siasa zisizoitakia mema nchi yao kutokana na tamaa binafsi  za baadhi ya wanasiasa ambazo  zimekuwa zikirudisha nyuma nchi yao  kimaendeleo  .

" SMZ  chini ya sera za CCM itaendelea  na mikakati  ya kuwatumikia wananchi  wote bila upendeleo  wa aina yoyote. Kazi ya kupeleka huduma muhumu za kijamii itasimamiwa na uongozi  wa  Rais Dk Mwinyi "Alieleza 

Hata hivyo  Mbeto aliwataka wananchi  wa  Pemba kuendelea kuiunga mkono serikali  yao ya awamu ya nane na ifikapo oktoba mwaka huu wajiandae kumchagua Rais,  madiwani, wawakilishi na wabunge toka CCM. 

'Wananchi wa pemba kinadharia na kiuhalisia wameamka na kutuma ujumbe mzito kwa upinzani .Muda na nyakati  zimebadilika. Pepo zinazovuma pemba ni mpya za wito wa  matumaini mapya kwa maendeleo "Alieleza Mbeto

Powered by Blogger.