CCM :Mapinduzi ya Zbar alama ya ukombozi


Na Mwandishi  Maalum , Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema haitoshi kukumbuka juhudi za ASP  zilizoiondoa ufalme wa  Zanzibar lakini wazanzibari wataendelea kuwaenzi  wote  waliojitolea kuikomboa nchi yao.

Katibu wa  Kamati Maalum ya NEC  Zanzibar  Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo, Khamisi  Mbeto  khamis ,amesema  Waafrika  wenyeji  wa Zanzibar  kabla  ya mwaka 1964 ,waliishi kwa madhila na  ukandamizaji wa haki  na kubaguliwa. 

Mbeto alisema  ASP    kiliwaongoza wazanzibari  bila kujali rangi zao, kabila ,asili na dini , walikataa kutawaliwa katika nchi  yao.

Alisema  wananachi hao chini  ya  uongozi wa Rais  wa ASP  Hayati  Mzee Abeid Amani Karume, kililazimika kufanya Mapinduzi  baada ya   watawala kuonekana hawako tayari  kukabidhi madaraka kwa njia ya uchaguzi.

'Wazee wetu  kwa kutekeleza  sera ,shabaha na malengo  ya ASP   toka  uchaguzi  mkuu wa kwanza mwaka 1957 kilishinda. Hata chaguzi  za 1961 na 1963 licha  ya ASP  kushinda hakikupewa utawala' Alisema Mbeto 

Aidha  Katibu  huyo Mwenezi  ,alisema  waafrika wa zanzibar  hawakuona njia mbadala ya kujitawala zaidi  ya  Mapinduzi yalioleta uhuru na mamlaka  kamili Zanzibar .

'Tutawaenzi  mashujaa wa Mapinduzi  waliojitolea muhanga kwa ajili ya  ukombozi  wa ndugu zao .Kwa  waliopoteza maisha yao kwa ajili ya kuikomba nchi  yetu mungu  aziweke roho zao mahali pema peponi "Alieleza 

Pia  Mbeto  alisema  baada ya miaka 61 kupita,  kizazi kipya cha wazanzibari  kitaendela kuyalinda na kuyaendeleza Mapinduzi hayo kwa gharama yoyote chini  ya uongozi  wa CCM na sera zake.

"Yote  yanayotekelezwa sasa na yajayo  chini ya SMZ    inayoongozwa na Rais  Dk  Hussein  Ali Mwinyi yanafuata   misingi  iliowekwa na ASP . Wanaodhani watayavuruga na kuivunja misingi ya Mapinduzi  hawataachwa watambe "alisisitiza Mbeto 

Vile vile  Mwenezi  huyo alisema jukumu la kuyalinda Mapinduzi  ni kiapo cha utii kwa kila mzanzibari aidha awe ni mwana CCM, ACT, Chadema au chama chochote .

Powered by Blogger.