YAS TANZANIA: YAFUNGA MWAKA KWA TUZO YA PILI, MTANDAO WENYE KASI ZAIDI TANZANIA: OOKLA 2024.

Waswahili husema nyota njema huonekana Asubuhi husemi huu umedhihirika Leo baada ya Kampuni ya Mawasiliano ya YAS Tanzania imeshinda Tuzo ya kuwa kampuni namba moja ya Mawasiliano yenye mtandao wa Internet wenye kasi zaidi " Ookla Speed test Award for the Fastest mobile network in Tanzania kwa mara ya pili mfulululizo.
ambapo kampuni ya YAS imeibuka mshindi wa kwanza kwa mwaka 2024 nakuziacha mbali kampuni zingine zinazotowa huduma ya mawasiliano nchini

Akizungumza wakati wa kutangazwa kwa ushindi huo hii leo Desemba 10,2024 Jijini Dar es Salaam, Kaimu CEO wa kampuni ya YAS Tanzania, Bw Jerome Albou, amesema wamekuwa washindi wa tuzo hiyo kwa Mwaka wa pili mfululizo na kwamba Yas Tanzania imepiga hatua kubwa sana kwenye kutoa huduma ya Internet yenye kasi zaidi nchini hivyo kukidhi vigezo vya kikataifa.

Aidha Albou amesema Kampuni ya YAS Tanzania Imewekeza Zaidi Shilingi Trioni 1 za kitanzania katika kuhakikisha Tanzania bara na Tanzania Visiwani inakuwa na minara 4000 ya kiwango cha 4G huku wakiifikidha 5G kwenye miji yote mikubwa Tanzania
Ameongeza kuwa wanapo wakati sherehekea ushindi huu wa Tuzo kutoka OKLA bado wanazingatia jukumu lao la kutoa huduma bora katika sekta ya Teknolojia ya Mawasiliano nchini, nakwamba wamejiwekea malengo madhubuti ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa Mtandao imara na kuleta mapinduzi katika sekta ya Digitali.
Akiwasilisha Ripoti ya ushindi wa YAS Tanzania , Osma Nawayse , kutoka Ookla amesema, kampuni ya Yas Tanzania imeshinda kwa asilimia 68.81 kwakuwa na Internet yenye kasi zaidi na hakuna kampuni yoyoye ya Mawasiliano Tanzania imefikia kiwango hicho.

Kwaupande wa Medium dowloder speed YAS Tanzania, imepata asilimia 43 ikizitangulia kampuni zote za Mawasiliano nchini Tanzania sambamba na kuongoza katika vipengele vingine tofauti tofauti kuusiana na masuala ya upatikanaji wa Internet yenye kasi zaidi nchini Tanzania.
Itakumbukwa kuwa Yas imebadili CHAPA mapema mwezi uliopita Kutoka kuitwa TIGO Tanzania ambapo sasa inajulikana kama YAS Tanzania ambapo pia, imebadili Jina la Tigo pesa ambapo sasa inajulikana kama Mixx by Yas, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Yas amesomba watanzania kuendelea kutumia huduma zinazozalishwa na Kampuni hiyo.


(Pichani) baadhi ya wanahabari na wafanyakazi wa kampuni ya Mawasiliano ya YAS Tanzania wakiwa kwenye Sherehe ya kukabidhiwa kwa Tuzo ya Ookla iliyofanyika Leo Desemba 10,jijini dar es salaam.

Powered by Blogger.