WAFANYAKAZI WA YAS TANZANIA WAIPAISHA CHAPA MPYA KILELENI, MLIMA KILIMANJARO
Na. Jumanne Magazi
7.12.2024
Moshi, Kilamanjaro
Wafanyakazi wa kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya YAS Tanzania wamefanya Utalii WA NDANI kwa kupandisha chapa mpya ya kampuni hiyo ya YAS Tanzania katika mlima Kilimanjaro.
Katika kile kinachoonekana kuongeza thamani ya kile unachokifanya kuwa Bora Zaidi.
Akizungumza wakati wa kupanda mlima huo,Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa kampuni hiyo, Bw. Henry Kinabo Amesema,Mazingira mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yameiwezesha Yas Tanzania kujidhihirisha kama mwekezaji kinara katika sekta ya mawasiliano nchini.
Kinabo alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuwakaribisha wafanyakazi 16 wa Yas Tanzania waliopanda Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kubadilisha nembo.
Awali aliwasifu wafanyakazi wa Yas Tanzania kwa kujituma, akisema mafanikio ya kampuni hiyo kushinda tuzo nyingi yamechangiwa na ubora wa huduma zake.
Katika safari hiyo,Washiriki wote 16, wakiwemo wanawake watatu, walifanikiwa kufika kilele cha Uhuru na kupandisha bendera za Yas na Mixx by Yas kwa fahari kubwa.
Katika hatua nyingine,Uzoefu wa Washiriki
Washiriki walielezea kupanda mlima huo kama tukio lenye changamoto lakini lenye kufurahisha. Bi. Evelyn Gamasa, mfanyakazi wa Yas, alielezea tukio hilo kama la kihistoria na kuwataka Watanzania kuthamini utalii wa ndani.
Naye Kiongozi wa safari hiyo, Bw. Emmanuel Mallya, ambaye ni Afisa Mkuu wa Ufundi wa Yas Tanzania, ameelezeaa dhamiya yao kuwa ni kuonyesha mafanikio yao kwa wafanyakazi hao katika kupanda mlima yameonyesha azma yao ya kuboresha huduma kwa wateja.
Post a Comment