CHIKU RASHID AFUNGA MWAKA NA MIL 1 YA "MAGIFT YA KUGIFT" DROO YA 7 KUTOKA: MIXX BY YAS 2024

Na Jumanne Magazi 

27.12.2024

Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya YAS, ikishirikiana na kitengo cha Mixx by Yas ,Leo hii Disemba 27,2024, imekabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi 7 wa Shindano la “Magift ya kugift” kwa wiki ya 7 ambapo kati ya hao 7  wamejishindia kiasi cha Shilingi Milioni 1 kila mmoja 

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Bidhaa kutoka Kampuni ya Mtandao wa simu wa Yas Eginga Mohameda amesema anayofuraha kuona wanakabidhi zawadi kwa washindi kwa wiki ya Saba 7, nakudai kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wao kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyinginezo katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka.

Eginga amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya  kiasi cha  TSh milion 180 kwa washindi wa makundi  tofauti ikiwemo,mawakala,na wateja wengine.

Kwa upande wake mshindi wa wiki hii akiwakilisha wenziwe Sita Chiku ambaye amejinyakulia kiasi cha Shilingi mil 1  “amemshukuru Yas kwa  kuchezesha kampeni hiyo ya "MAGIFT ya KUGIFT 2024" na hatimaye yeye kuibuka mshindi, na amewaomba watanzania kushiriki kampeni zinazoletwa na Yas Tanzania kwani hakuna ubabaisha kila mtu anashinda kutokana na BAHATI yake amesema Chiku.


Kampuni ya YAS imekuwa na muendelezo mzuri WA kuendesha kampeni mbalimbali ikiwa sehemu ya kujitangaza itakumbukwa kuwa kampuni ya YAS ilizinduliwa hivi karibuni ikichuka pahala la Tigi ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka 30 ikitoa huduma zake hapa nchini, na kutunukiwa Tuzo mbali mbali ndani na Nje ya nchi, ikiwemo Tuzo ya mtandao wenye Kasi Zaidi Barani Africa inayotolewa na OOKLA.

Hii ni wiki ya Saba  mfulululizo kati kati ya wiki 12 ambazo Yas kupitia msimu huu wa siku kuu, ikishirikiana na kitengo cha Mixx by Yas,  imeendelea kutoa zawadi Zaidi kupitia kampeni Yao ya "Magift ya kugift" kwa wateja wao kwa mwaka huu wa 2024.


Powered by Blogger.