UZINDUZI WA KAMPENI YA SERIKALI ZA MITAA PWANI WATUMA SALAMU MAHSUSI KWA VYAMA VYA UPINZANI
Ndugu Jokate Urban Mwegelo (MNEC), Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM amezindua Rasmi kampeni ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji ndani ya Kata ya Bungu, Wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani.
Ndugu Jokate alizindua Rasmi kampeni hiyo kwa kuhamasisha WanaCCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo.
Ndugu Jokate katika hotuba yake alihimiza zaidi juu ya ushirikiano, umoja na mshikamano katika kutafuta ushindi wa kishindo kwa CCM, hii ni pamoja na kuwasihi kuzingatia Tamko la Uchaguzi lililotolewa kama dira kulekea tarehe 27 Novemba, 2024.
Pamoja na mambo mengine aliendelea kuwasisitiza wana Kibiti kuendelea kumuunga Mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna alivyoweza kuitekeleza Ilani ya CCM ya 2020/25 na anavyoendelea kukiongoza Vyema Chama Cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla.
Post a Comment