AIR FRANCE KLM: YAZINDUA SAFARI- YA PARIS,KILIMANJARO MARA 3 KWA WIKI
Na. Jumanne Magazi
20.11.2024
Shirika la ndege la Ufaransa, Air France KLM kwa mara ya kwanza imezindua safari mpya ndege hiyo, ambayo itakuwa ikianzia Paris Nchini Ufaransa na kuja Kilimanjaro, Kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumza kwenye Halfa ya uzinduzi huo, Naibu Waziri WA uchukuzi Mh David David Kihenzile, amesema uzinduzi huo ni sehemu ya mafanikio kama nchi katika Sekta usafiri WA anga lakini pia katika ukuaji WA uchumi Kupita Utalii hususani kwa Kanda ya kaskazi uzinduzi uliofanyika kwenye uwanjani wa ndege WA kimataifa wa Kilimanjaro.
Naye Meneja mkuu wa Air France KLM anayesimamia Kanda ya mashariki kusini mwa Afrika pamoja na nchi za Nigeria na Ghana, Marius van der Ham, amesema wanayofuraha kuanzisha safari hiyo kwani inakwenda kuleta matokeo makubwa kwao kama shirika la ndege.
Aidha ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya a uchukuzi kukubali kuanza kwa safari hiyo kupitia ndege Yao aina ya Airbus A350-900, ambayo inauwezo kusafiri Eno kubwa barani Ulaya ambayo ni ndege kubwa na kongwe katika Biashara ya anga na hatimaye kuja hapa Tanzania.
Wakati huo huo Meneja WA Air France - KLM's Nchini tanzania Tanzania Country Rajat Kumar, akitoa Salamu wakati WA Uzinduzi huo amesema kwa uzoefu WA shirika Hilo kupitia ushirikiano baina ya tanzania Tanzania na Ufaransa ambapo amesema kuanzishwa kwa safari hiyo kuongeza udugu na uhusiano huo wa muda mrefu
Aidha Kumar amefafanua kuwa ndege hiyo itakuwa ikitua katika uwanjani WA ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ambako ndipo kulipofanyika uzinduzi huo.
Post a Comment