OYA YALAANI VIKALI TUKIO KUSIKITISHA LILOFANYWA NA MAOFISA WAKE KUSABABISHA KIFO
Na JUMANNE MAGAZI
Dar es salaam
Kampuni ya OYA Microfinance imelaani kitendo kilichofanywa na maafisa wake ya kumpiga hadi kumsababishia kifo mkazi wa mlandizi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani Juma Mfaume tukio ambalo limetokea Oktoba 07,2024.
Katika taarifa yake kampuni hiyo imeeleza kusikitishwa kwake kuhusu tukio hilo huku ikieleza kuwa kampuni hiyo haijawahi kuidihinisha wala kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake kutumia nguvu katika urejeshaji wa madeni.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa kampuni hiyo inafanya kazi kwa kuzingatia sheria na maadili huku tukio hilo halionyeshi maadili wala taratibu za kazi zao.
Itakumbukwa kuwa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani lilitoa taarifa juu ya kukamatwa kwa wafanyakazi wanne wa kampuni ya OYA ambao wamehusika na mauaji hayo.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa makampuni na taasisi za kifedha kufuata taratibu za kisheria katika kudai fedha kutoka kwa wateja wao ili kuepusha usumbufu na madhara yanayoweza kutoka ikiwemo uharibifu wa Mali, kujeruhi na vifo.
Post a Comment