WANAFUNZI 1,633,900, WASAJILIWA KUANZA MTIHANI WA MAJARIBIO DARASA LA NNE 2024, KESHO TANZANIA BARA
Baraza la mitihani Nchini NECTA, limesema jumla ya wanafunzi 1,633,900 Nchini wamesajiliwa tayari kwa kufanya mtihani WA kujipima WA darasa la nne kuanzia kesho tar 23 hadi 24, mwaka 2024.
Akiongea na Waandishi wa habari hii Leo Oktoba 22,2024, Katibu Mtendaji wa Baraza Hilo, Said A Mohamed, amesema tayari jumla ya shule za msingi 20,069 kote Tanzania bara zimethibitishwa kuwa vituo vya mtihani huo WA kujipima wa darasa la nn
e.
Kwa upande mwingine Mohamed amesema kuwa ametangaza kuanzia Oktoba 28,hadi Novemba 7 2024, ndio utafanyika mtihani WA kujipima kwa wanafunzi WA kidato cha pili,(FTNA) mtihani ambao utafanyika katika shule 6617 Tanzania bara.
Aidha amesema dhana ya upimaji wa kitaifa hutofautiana na ile ya mitihani ya Taifa kwa upimaji hufanywa katika mafunzo wakati mitihani ya Kimataifa hufanywa mwishoni mwa mafunzo.
Katika hatua nyingine Bw Mohamed amefafanua kuwa kati ya hao wavulana ni 794,021, sawa na asilimia 48.60 ambapo wanaume ni 839879 sawa na asilimia 51.40.
Wanafunzi WA kidato cha pili:
Kwa upande wa watahiniwa WA kitadato cha pili shule 869673 waliosajiliwa kati Yao wavulana ni 399383 sawa na asilimia 45.92. huku wasichana wakitaraji wakiwa 470290 ambao ni sawa na asilimia 54.08.
Kwa upande wa wanafunzi WA kujitegemea 9618 waliosajiliwa wavulana ni 3712 sawa na asilimia 38.59 na wasichana ni 5906 ambao ni sawa na asilimia 61.41 aidha pia amesema wapo wanafunzi 66 wenye nahitaji maalum kati Yao wenye uoni hafifu ni 65 na asiyona ni 1.
Mohamed ametoa wito kwa wasimamizi wote walioteuliwa kusimamia upimaji huo kufanya kazi Yao kwa umakini na uadilifu WA hali ya juu.
Kwa upande mwingine Kaimu huyo ametoa wito kwa wanafunzi kutofanya hila mbinu za aina YOYOTE kwenye kipindi cha mitihani hiyo ya kujipima vinginevyo taratibi na Sheria zote zitachukuliwa dhidi Yao kwa atakayebainika kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na taratibu za mitihani ambapo Ameongeza kuwa Baraza la mitihani Tanzania halitasita kuchukua hatua Kali za kisheria ikiwemo kufuta matokeo Yao.
Post a Comment