TIGO YAANZISHA MFUMO MPYA WA ULIPAJI TIKETI ZA TRENI YA SGR
Na. Jumanne Magazi
08.10.2024
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Nchini ikishirikiana na Shirika la Reli Tanzania TRC leo Oktoba 8 2024, imezindua mfumo wa kisasa wa ulipaji wa tiketi za SGR wenye lengo la kurahisisha ulipaji wa tiketi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi pamoja na makubaliano ya ushirikiano baina ya Tigo na TRC, Afisa mkuu wa Tigo pesa Bi Angelika Pesha amesema tigo inayofuraha kuingia makubaliano na TRC kupitia treni yake ya mwendokasi yaani SGR hivyo huu ni mwanzo mzuri mafanikio ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikitoa huduma zake Nchini kwa kipindi cha miaka 30 sasa
Aidha Kadogosa ameendelea kusisitiza kuwa wao kama shirika ni wajibu wao kuandaa Mazingira mazuri ya ufanyaji kazi ikiwemo kujenga miundombinu ya treni hiyo hivyo baada ya kukamilika sasa wanataka kupanua wigo wa utiaji huduma zake kwa Wananchi ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa tiketi za SGR.
Naye Meneja wa huduma kwa wateja TRC, Bi Catherine Moshi amemshukuru kampuni ya Tigo kuingia makubaliano Shirika Hilo kwani wao kama watendaji na watoa huduma kila siku itawarahisishia kufanya kazi kwa unafuu ili kuwapunguzia usumbufu WA kupanga foleni kwenye stesheni za Reli badala yake Wananchi watakuwa na fursa ya kukata tiketi kupitia simu zao mkononi.Uzinduzi mfumo huo wa malipo ya SGR ulitanguliwa na matukio mbalimbali ikiwemo TRC kutoa Tuzo na zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi, Taasisi mbalimbali za kisekta pamoja na wadau treni ya SGR, hiyo ikienda sanjali na wiki ya huduma kwa mteja ambayo kampuni Tigo na TRC wakiwa WATOA huduma kwa jamiii Nchini.
Post a Comment