MCHAKATO TUZO ZA "SAMIA KALAMU AWARDS" WASOGEZWA MBELE HADI OCT 30 MWAKA HUU
Na JUMANNE MAGAZI
24.10.2024
Katika kile kinachoonekana kujali na kutambua thamani na Kazi na wanahabari hapa Nchini.
Waandaaji wa tuzo za habari za maendeleo zijulikanazo kama 'Samia Kalamu Awards' wameongeza muda wa kuwasilisha kazi hadi Oktoba 30 mwaka huu ilo kutoa nafasi ya waandishi wengi zaidi kushiriki.
Tuzo hizo zilizozinduliwa rasmi Oktoba 13,2024 zinaandaliwa kwa ushirikiano wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Akizungumza leo Oktoba 24,2024 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dk. Rose Reuben, amesema awali tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ilikuwa Oktoba 26 lakini wameongeza muda hadi Oktoba 30,2024.Amesema uamuzi wa kuongeza muda umechukuliwa ili kutoa nafasi kwa wale waliokutana na changamoto za kiufundi ikiwemo kushindwa kupandisha kazi mitandaoni kutokana na matatizo ya mtandao na changamoto nyingine.
Amesema mpaka sasa wamepokea maombi 250 kutoka mikoa 23 ya Tanzania Bara na kusisitiza kuwa kazi zinazowasilishwa zinatakiwa kuwa za kipekee na ambazo hazijawahi kuwasilishwa kuwania tuzo nyingine na zinazofuata taratibu za haki miliki.
Tuzo hizo zinalenga kuhamasisha, kukuza na kupanua wigo wa uandishi, utangazajo na uchapishaji wa maudhui ya ndani kupitia vyombo vya habari vya asili na mitandaoni ili kuchochea uandishi wa makala za kina zinazozingatia maendeleo, uwajibikaji, mila na tamaduni pamoja na kujenga chapa na taswira ya nchi.
Nao baadhi ya wadau wameonyesha kuhamasika na Tuzo hizo ambapo wameomba Zoezi Hilo liwekwe kwenye karenda ya Tamwa, ili kuleta tija kwa wanahabari na Taifa kwa ujumla.

Post a Comment