LATRA, CCC, NA FCS ,WASAINI DILI LA MIAKA 3 KULINDA HUDUMA WATUMIAJI HUDUMA ZA ARDHI
22.10.2024.
Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri wa ardhini kutoka LATRA kwa kushirikiana na Shirika la Asasi za Kiraia nchini (FCS), wamesaini mkataba wa makubaliano ya miaka mitatu ya programu itakayowezesha kulindwa kwa haki za mtumiaji wa barabara, reli na waya.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano hayo leo Oktoba 22, 2024 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Justice Rutenge amsema ushirikiano huo ni wa muhimu katika kuchechemua uwakilishi wa wananchi na kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watumiaji.
"Kujitolea kwetu kwa ulinzi wa watumiaji kunatokana na dhana ya msingi ya haki muhimu za watumiaji, ikiwa ni pamoja na haki ya malipo ya madai, elimu ya udhibiti wa usafirishaji wa bidhaa na huduma za ardhini," amesema
Rutenge.
Ameeleza kuwa, LATRA CCC ni mdau muhimu wa maendeleo ya ulinzi wa watumiaji katika sekta ya usafiri wa nchi kavu, hivyo kupitia ushirikiano huo FCS itaongeza ujuzi wa kujenga uwezo wa kutekeleza mipango inayolenga kulinda haki za watumiaji nchini.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa LATRA CCC, Daud Daud amesisisitiza umuhimu wa ufumbuzi wa changamoto na ushirikiano miongoni mwa wadau wa maendeleo wakati Tanzania inaelekea kukuza mazingira yanayounga mkono haki za mlaji.
"Ushirikiano kati yetu ni mfano wa juhudi za pamoja za kukuza mazingira ya biashara ya usawa na kuwawezesha watumiaji ujuzi kutambua haki zao na chaguzi sahihi za usaidizi." Amesema Daud.
Naye Mkuu wa Programu FCS, Nasim Losai amebainisha kuwa LATRA CCC ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria na. 3 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), Kif. cha 29 ya mwaka 2019. Hivyo, ushirikiano huo utaongeza chachu ya kutambulika majukumu yake zaidi kwa jamii.
Post a Comment