KITANDULA ASIFU JUHUDI ZA UWEKEZAJI SEKTA YA UTALII
12 Okt.2024
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dastan Kitandula amesema kuwa, kutokana na uwekezaji mzuri wa miundombinu rafiki katika sekta ya utalii imechangia kwa kiasi kikubwa kuwavutia watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza nchini Tanzania.
Ameitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa jukwaa la uwekezaji katika sekta ya Utalii Nchini Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam,ikiwa ni sehemu ya onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Kiswahili( S!TE) 2024.
Aidha Kitandula amesema kuwa sekta ya Utalii inaingiza fedha nyingi za kigeni,pamoja na kuchangia kiasi kikubwa katika pato la Taifa( DGP) hivyo Serikali itaendelea kuweka jitihada za msingi katika kuimarisha uwekezaji kwenye sekta hiyo ili kukuza uchumi.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii Nkoba Mabula amesema kwamba,zipo fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya utalii nakuwasihi watu wote wanaohitaji kuwekeza wafike katika Ofisi za mamlaka za uwekezaji ikiwemo Kituo Cha uwekezaji Tanzania( TIC) na Kituo Cha uwekezaji serikali ya Mapinduzi Zanzibar (ZIPA) ili waweze kupata taratibu hizo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania( TTB) Ephraim Mafuru amesema kuwa lengo la onesho hilo ni kuwakutanisha Watoa huduma waliopo katika mnyororo wa thamani wa Utalii Ndani na nje ya Nchi ambao watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao za Utalii na kutengeneza Mtandao wa Biashara( Business Network)
Amesema onesho hilo linaenda sambamba na Utekelezaji wa sera ya Taifa ya Utalii ya Mwaka 1999 pamoja na mkakati wa kutangaza Utalii Kimataifa ( 2020-2025 ) ambayo imetilia mkazo kutangaza Tanzania kama kivutio Bora cha Utalii Duniani.
Post a Comment