TTB YAWAITA WADAU WA UTALII KUCHANGAMKIA FURSA KWENYE ONESHO LA S!TE 2024
Na. JUMANNE MAGAZI
Hatimaye Bodi ya Utalii Tanzania TTB imezindua rasmi Onesho la nane la Swahili International Tourism Expo _S!TE (S!TE 2024) ambalo linatarajia kufanyika Octoba 11 hadi 13 Jijini Dar es salaam.Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 12, 2024 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Ephraim Mafuru amesema lengo la onesho hilo ni kuwakutanisha watoa huduma waliopo katika mnyororo wa thamani wa utalii kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema Onesho hilo litakwenda sambamba na utekelezaji wa sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 pamoja na mkakati wa kutangaza utalii kimataifa (2020-2025) ambayo imetilia mkazo kuitangaza Tanzania kama kivutio bora cha utalii.
“Onesho hili pia ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano III( FYDP III 2021/22_2025/26 ambalo zao la utalii wa mikutano na matukio (MICE Tourism) limeanishwa kama zao la utalii la kimkakati kwa lengo la kufikia watalii millioni tano na mapato ya Dola za Marekani Billioni sita ifikapo mwaka 2025,” amesema.
Aidha amesema Onesho hilo linatarajia kuhudhuriwa na waoneshaji wa bidhaa na huduma za utalii zaidi ya 120 sambamba na wanunuzi wa bidhaa na huduma za utalii (International Hosted Buyers) takribani 120 kutoka Nchi ambazo masoko ya kimkakati ya utalii ikiwemo Asia, Ulaya na Amerika.
Ameongeza kuwa, Onesho hilo litahusisha utangazaji wa bidhaa mbalimbali za utalii, jukwaa la uwekezaji, semina kuhusu masuala ya utalii na masoko na mikutano ya wafanyabiashara za utalii.
Post a Comment