TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA WAWEKEZAJI WA MADINI NOV 19 HADI 21 MWAKA HUU.

Waziri wa Madini Mh Antony Mavunde amezindua Rasmi maandalizi ya Mkutano wa wawekezaji katika Sekta ya Madini hapa nchini, ambao umepangwa kutafanyika kuanzia November 19 hadi 21 mwaka huu Jijini dar es salaam.

Akizungumza kwenye kongamano maalum lililoandaliwa kwa pamoja kwa kushirikiana na Chemba ya madini ambao ndio Waandaaji wa kongamano hilo.

Amesema mkutano huo unalenga kuwakutanisha wadau na wawekezaji Kutoka sehemu mbalimbali za Dunia ambao watakutana Nchini kwa lengo la kubadirishana mawazo lakini pia kuongeza mnyororo wa thamani katika Sekta ya madini.


 Naye katibu mkuu wa Tanzania Chembers of Minings, Eng Benjamin Mchwampaka amesema mkutano huo utakuwa ni sehemu muwafaka kwa wadau wa uwekezaji katika Sekta ya madini ambao watakutana KUJADILI na kupeana uzoefu na utaalamu katika kuongeza mnyororo wa thamani wa madini yanayopatikana hapa nchini wenye lengo la kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Aidha Mchwampaka amesema wao pamoja na Serikali wameshirikiana kuandaa Mkutano huo ili kuangalia kwa karibu Sera, Sheria ,kanuni zilizowekwa zinaweka Mazingira mazuri katika uwekezaji ili kuleta tija kwa pande zote na kusaidia ukuweji wa Sekta hiyo muhimu ambayo inatajwa kuchangia asilimia 9 ya pato la Taifa.


Powered by Blogger.