TALGWU YAISHUKURU SERIKALI KUSIKIA KILIO CHAO NA KUANZA KULIPA MISHAHARA KUPITIA HAZINA


 Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimeipongeza hatua ya Serikali ya kuridhia ombi lao la muda mrefu la kutaka kuwalipwa kwa Wanachama wake kupitia Mfuko Mkuu wa Serikali (HAZINA).

Akizungumza mapema leo Agoust 14,2024 jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa TALGWU, Bw. Rashidi Mtima wakati amesema tayali wanachama 465 kati ya 645 wameshaanza kulipwa kupitia HAZINA, kuanzia Julai 2024 tofauti na hapo awali ambapo walikua wakilipwa kupitia mapato ya Ndani ya Halmashauri.

"TALGWU tunaipongeza serikali kwa hatua hiyo kwani itasaidia kuondoa kero ya muda mrefu na kuongeza Ari na Morali ya kufanya kazi kwa watumishi hao ikiwa ni pamoja na kuondokana na Changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili awali'. Alisema Bw. Mtima

Amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kutolipwa mishahara kwa wakati, kukosa huduma za Matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutokana na makato kutowasilishwa kwa wakati.

Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni kutokukopesheka katika baadhi ya taasisi za Fedha,kupata usumbufu mkubwa kipindi watumishi wanapostaafu kutokana na makato ya michango yao kutokuwasilishwa kwa wakati katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii( NSSF).

Aidha bwana Mtima aliongeza kuwa pamoja na pongezi hizo tunaiomba Serikali kufanya mchakato ili wanachama wetu 180 waliosalia ambao bado wanalipwa kwa kupitia mapato ya Ndani ya Halmashauri nao waanze kulipwa kupitia Hazina.

Alisema katika kipindi hiki ambacho Serikali inashughulikia maombi ya watumishi walio salia nao kuanza kulipwa na HAZINA, nitoe wito kwa Serikali kuhakikisha kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri husika wanalipa mishahara kwa wakati kama ambavyo inafanya HAZINA.

Katika hatua nyingine Bw. Mtima

amezitaja Halmashauri ambazo bado zinalipa kupitia mapato ya Ndani ni Geita Mji,Ilala Jiji,Manispaa ya Kinondoni,Mbeya Jiji, Jiji la Mwanza, Manispaa ya Temeke, Dodoma Jiji na Manispaa ya Morogoro, na kuzitaka kulipa mishahara ya Watumishi hao kwa wakati.

Chanzo (harakati za Jiji blog)

Powered by Blogger.