TANZANIA KUZINDUA SERA YAKE YA VIWANDA NA BIASHARA
Akizungumza mbele ya waandishi WA habari hii Leo Waziri wa Viwanda na Biashara Selemani Jafo amesema sera hiyo inalengo la kuweka mfumo na mikakati madhubuti wenye lengo la kuboresha Mazingira ya Biashara ukienda sambamba na ukuaji WA uchumi endelevu.
Aidha Jafo amesema washiriki wapatao 300 wanatazamiwa kushirikiana uzinduzi huo ikiwajumuisha wadau mbalimbali Kutoka Taasisi za umma, Taasisi binafsi, mashirika ya Dini, wabia wa maendeleo, mabalozi,vyama vya wafanyabiashara na wenye viwanda na Biashara.
Lakini baada ya Azimio la Arusha mwaka 196, Shughuli za uchumi ikiwemo Biashara za jumla mauzo ya Nje ya nchi pamoja na uagizaji WA bidhaa ziliendeshwa na Taasisi za Umma.
Vilevile Waziri Jafo hakuacha kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana kupitia Utekelezwaji WA sera ya Taifa ya Biashara ya mwaka 2003.
Vilevile Waziri Jafo hakuacha kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana kupitia Utekelezwaji WA sera ya Taifa ya Biashara ya mwaka 2003.
Ambapo amesema Serikali umefanikiwa kushiriki kikamilifu katika majadiliano mbalimbali ya Biashara baina ya nchi na Nchi.
Ikiwa sambamba na jumuiya mbalimbali za kikanda pamoja na kupata fursa za biashara kwenye Kanda hizo ambapo amezitaja baadhi ya Kanda hizo zikiwemo EAC,SADC,AFCFTA, pamoja na masoko mbalimbali ya biashara Kutoka Nchini China
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Trade Mark Africa Bw Elibariki Shammy ameipongeza Wizara ya viwanda na Biashara kwa hatua, hiyo kubwa ya kuzindua sera ya Taifa ya Viwanda na Biashara kwani huo ni muelekeo mzuri kwa. Taifa katika kukupa kiuchumi, pamoja na kuweka Mazingira Bora kwa wawakezaji katika Sekta ya Viwanda na biashara hapa Nchini.
Post a Comment