SGR YAANZA RASMI SAFARI DAR KWENDA DODOMA


Hatimaye Safari ya Treni ya Mwendokasi SGR, Kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma imeanza Rasmi Leo alhamis Julai 25 2024 saa 12 Asubuhi.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema kabla ya kuanza kwa safari hiyo. Mkurugenzi mkuu wa Shirika Hilo Masanja Kungu Kadogosa amesema kuanza kwa safari hiyo ni muitikio wa kauli ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ambaye aliagiza ifikapo julai mwaka huu safari ya Treni hiyo iwe imeanza. Kadogosa amesema Zaidi ya abiria 900 wamesafiri kwenye treni hiyo iliyokuwa na mabehewa 14.

Katika hatua nyingine Kadogosa amesema safari Rasmi itatangazwa Baadae baada ya Kupata uhakika WA Mgeni Rasmi ambaye anategemewa kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan na ameahidi kuongea na wanahabari ndani ya siku mbili zijazo.
Vilevile Kadogosa amezungumzia muitikio wa watu ambapo amesema muitikio ni mkubwa katika kukata tiketi ikenda sambamba na kufuata utaratibu ulioandaliwa.
Kwa upande wake Zakaria daudi mukti ambaye ni mmoja wa abiria ambaye amesafiri na treni hiyo amesema kuwa kwa upande wake ameridhika na amefurahia kusafiri na treni hiyo ikiwa ni safari yake ya kwanza Kutoka Dar es salaam hadi Dodoma.
Naye Jesca mchau mkaazi WA Dar es salaam amesema yeye kwake ni mara ya kwanza kusafiri na treni hivyo ni furaha kubwa kwake kuwa sehemu ya miongoni mwa abiria WA kwanza kusafiri na treni hiyo.


 

Powered by Blogger.