KADI ZA ZAMANI ZA MPIGA KURA NI HALALI: TUME

Kadi za mpiga kura zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 ni halali na zitaendelea kutumika kwenye chaguzi kuu zijazo bila kujali mabadiliko ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Akizungumza wakati wa ziara aliyoifanya ya kukagua vituo vya kuandikishia wapiga kura leo tarehe 22 Julai, 2024 katika

Halmashuari ya Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan amesema wapiga kura wenye kadi hizo hawahusiki na zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

“Naomba nitoe wito kwa wale ambao kadi zao ni zile zenye jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wanadhania kuwa kubadilika kwa jina la Tume kunasababisha kubadili kadi watambue kuwa kadi zao ni halali kwa mujibu wa kifungu cha 168 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024,” amesema. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan (kulia) akizungumza na Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kasulu Vijini, Bw. Emmanuel Ladislaus alipofika kwenye ofisi za afisa mwandikishaji huyo kwa ajili ya kufanya ziara ya kukagua vituo vya kuandikisha wapiga kura. 

3-10: Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan akiwa kwenye ziara ya kukagua vituo ambapo kwenye baadhi ya maeneo aliagiza kuongezwa kwa BVR Kit kutokana na hamasa kubwa ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha na wapiga kura waliojitokeza kuboresha taarifa zao.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan akiwa kwenye ziara ya kukagua vituo ambapo kwenye baadhi ya maeneo aliagiza kuongezwa kwa BVR Kit kutokana na hamasa kubwa ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha na wapiga kura waliojitokeza kuboresha taarifa zao.

 

Powered by Blogger.