DIWANI KIMWANGA: AWATAKA WAZAZI KUPUUZIA TAARIFA ZA UZUSHI KUPOTEA KWA WATOTO MASHULENI
Na Jumanne Magazi
Diwani wa kata ya makulumla wilaya ya Ubungo,jijiji Dar es salaam,Bakari Kimwanga, amesema kumekuwa na taarifa nyingi zinazo husiana na kutekwa kwa watoto wakiwa mashuleni ambapo amesema taarifa hizo kuwa sio za kweli.Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara maalum uliofanyika katika shule za msingi za Dr. Omar Ali Juma na Karume uliowakutanisha viongozi wa kiserikai na chama wazazi walimu kamati ya ulinzi na Usalama wakiwemo wadau wa Elimu Kutoka kata ya makurumla.
Amesema "wazazi mnatakiwa kuacha kuacha kuzua taharuki pindi mnaposikia uzushi unaozagaa kuhusiana na kutekwa au kuuwawa kwa watoto pindii wanapokuwa shuleni"
Kwa upande wake mwenyekiti wa Usalama kata ya makulumla afande Emanuelamewahakikishia wazazi na walezi kuwa hali ya Usalama ya watoto wao katika kata ya makulumla huku akiomba ushirikiano uendelee baina ya wazazi walezi KAMATI za shule Serikali na jamii kwa ujumla.
Post a Comment